Shirika La AGPAHI Lakabidhi Vifaa Vya Kutolea Elimu Ya Ukimwi na Michezo Kwa Klabu Za Vijana Wanaoishi Na VVU Shinyanga


Hapa ni katika ukumbi wa Vigirgmark Hotel mjini Shinyanga ambapo siku ya Ijumaa,Aprili 15,2016 ,Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids HealthCare Initiave( AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi limekabidhi vifaa vya kuwezesha kutoa elimu zaidi kwa vijana juu ya afya ya uzazi na burudani.


Vifaa hivyo vilivyotolewa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Mfuko wa kusaidia watoto wa Uingereza (Children's Investment Fund Foundation UK-CIFF), ni kwa ajili ya klabu za vijana katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala,Manispaa ya Shinyanga na Kahama Mji.

Vifaa vilivyokabidhiwa katika klabu za vijana za wilaya tajwa hapo juu ni runinga (Tv), Deki (DVD Player), redio (Subwoofer systems), Flash Disc, Marker pens ,Flip charts,Rim papers,kalamu,penseli za kuchorea,vifaa vya michezo zikiwemo jezi ,viatu na mipira.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo,Meneja miradi wa Shirika la AGPAHI Dr. Gastor Njau,mbele ya mgeni rasmi kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa alisema vifaa hivyo vimenunuliwa chini ya ufadhiliwa na Mfuko wa CIFF kwa ajili ya kuwezesha kuwapatia elimu zaidi vijana juu ya afya ya uzazi.

Dr. Njau alisema vifaa hivyo vimegawiwa katika klabu 12 za vijana zenye jumla ya vijana 104 mpaka sasa.

"Tangu mfuko wa CIFF uanze ufadhili wake mkoani Shinyanga,mbali na kutoa ufadhili wa baiskeli 104 kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika halmashauri nne za wilaya hivi karibuni,pia umeanzisha klabu 12 ambapo 2 zipo katika halmashauri ya Mji wa Kahama,3 zipo Msalala,4 zipo Ushetu na 3 katika Manispaa ya Shinyanga",alieleza Dr. Njau.

Alisema vifaa hivyo vilivyogharimu zaidi ya shilingi milioni 20 vitatumiwa na vijana waliopo katika vituo vilivyopo kwenye halmashauri ya Ushetu ambavyo ni Zahanati ya Chambo,Kituo cha afya cha Ushetu,Ukune na Bulungwa.

Katika halmashauri ya wilaya ya Msalala ni kituo cha afya Chela,zahanati za Segese na Lunguya huku katika Mji wa Kahama ni zahanati ya Kagongwa na hospitali ya mji wa Kahama.

Dr. Njau alivitaja vituo vingine vilivyopata msaada katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kuwa ni kituo cha afya Kambarage na hospitali ya Kolandoto.

Aidha Dr.Njau alisema walengwa wa vifaa hivyo ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 ambao wapo katika rika balehe.

Aliongeza kuwa shirika linatambua kuwa kundi hilo ni muhimu sana katika jamii hivyo shirika linapenda kuona wanapata huduma rafiki za afya ya uzazi ikwemo habari na elimu sahihi.

"Baadhi ya vifaa mfano TV na DVD Player vitatumika kucheza mikanda yenye elimu mbalimbali kuhusu ujana pale vijana hawa wanapokutana kwa ajili ya kliniki ya afya kupata huduma",alisema Dr. Njau.

"Tayari tulishagawa mikanda ya kuelimisha vijana katika vituo vya Chela,Segese,Lunguya,Chambo,Ukune na Ushetu na tunaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha kuwa vituo vilivyobakia navyo vinapata mikanda hiyo mapema iwezekanavyo",aliongeza Dr. Njau.

Katika hatua nyingine Dr. Njau aliwaomba viongozi wa afya ngazi ya wilaya kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa na kuhakikisha vinatumika kwa ajili ya kuwaelimisha vijana hao na siyo vinginevyo.

Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa manispaa ya Shinyanga Dr. Laurent Mahembe alilipongeza shirika la AGPAHI kuwasaidia vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kama inavyotakiwa.

Kwa upande wao baadhi ya vijana waliopata vifaa hivyo(majina tunayahifadhi) walilishukuru shirika la AGPAHI kuwa kuwapatia msaada huo kwani kwa muda mrefu walikuwa na uhitaji wa vifaa hivyo ambavyo watavitumia kwa ajili ya kusambaza taarifa kwa jamii hususani katika vijijini

Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 28 hapa chini jinsi zoezi lilivyofanyika kuanzia mwanzo hadi mwisho mwa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo

Vifaa kwa ajili ya vijana (hawapo pichani kwa sababu ya maadili)katika klabu za vijana katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU katika halmashauri nne za wilaya mkoani Shinyanga.Vifaa hivyo ni runinga (Tv), Deki (DVD Player), redio (Subwoofer systems),Flash Disc,Marker pens,Flip charts,Rim papers,kalamu,penseli za kuchorea,vifaa vya michezo zikiwemo jezi ,viatu na mipira

Meneja miradi wa Shirika la AGPAHI Dr. Gastor Njau akizungumza wakati akikabidhi runinga (Tv), Deki (DVD Player), redio (Subwoofer systems),Flash Disc,Marker pens,Flip charts,Rim papers,kalamu,penseli za kuchorea,vifaa vya michezo zikiwemo jezi ,viatu na mipira kwa klabu za vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 wanaoishi na VVU katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala,Manispaa ya Shinyanga na  Kahama
Mji.
Dr. Njau akielezea namna vifaa hivyo vitakavyotumika kutoa elimu kwa vijana kuhusu afya ya uzazi na kuwapatia burudani

Vifaa vilivyotolewa kwa vijana hao

Dr. Njau akieleza namna shirika la AGPAHI linavyopambana na maambuzi ya VVU katika mkoa wa Shinyanga ambapo mbali na kugawa vifaa hivyo shirika hilo limekuwa likitoa elimu kwa watoa huduma ngazi ya jamii na misaada mbalimbali ikiwemo kutoa vifaa tiba katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU

Wawakilishi wa afya kutoka halmashauri za wilaya zinazofanya kazi wa shirika la AGPAHI wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akitafakari kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa halijaanza

Kushoto ni Afisa Mradi wa tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU kutoka shirika la AGPAHI Fidelis Temba akitafakari jambo wakati wa kugawa vifaa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia vijana wanaoishi na VVU.Kulia ni Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akijiandaa kukabidhi vifaa hivyo

Wawakilishi wa afya kutoka halmashauri za wilaya wakishuhudia zoezi la kukabidhi vifaa hivyo

Kushoto ni Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa kwa vijana

Tunashuhudia vijana wetu wakikabidhiwa vifaa.....

Kushoto ni Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akitoa maelezo kuhusu vifaa hivyo kabla ya zoezi la makabidhiano halijaanza,kulia kwake ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa

Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akibeba TV wakati wa makabidhiano hayo

Kushoto ni Afisa Mradi wa tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU kutoka shirika la AGPAHI Fidelis Temba na Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula wakiandaa vifaa hivyo wakati wa kukabidhi kwa vijana hao

Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akitoa redio kwenye boksi

Vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa kwa vijana (hawapo pichani)
 
Dr. Njau akikagua TV iliyokuwa kwenye boksi kabla ya kuikabidhi kwa wahusika
Kushoto ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya halmashauri nne za wilaya katika mkoa wa Shinyanga,na baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka AGPAHI alikabidhi kwa wawakilishi wa vituo vya tiba na matunzo vyenye klabu za vijana

Kulia ni Dr. Majigwa akizungumza wakati wa zoezi hilo la makabidhiano ambapo alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kutokana na jitihada wanafanya katika mapambano dhidi ya VVU katika jamii hususani kwa vijana,watoto na akina mama

Kushoto ni Afisa Mradi wa Watoto kutoka AGPAHI Julieth Kabengula akikabidhi moja ya TV kwa Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa (katikati) na kaimu mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dr. Laurent Mhembe (kulia)

Zoezi la makabidhiano linaendelea...

Kulia ni Dr. Njau akikabidhi TV kwa mwakilishi wa kituo cha Afya cha Kambarage kilichopo katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Dr.Laurent Mhembe (kulia),ambaye ni mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga

Kulia ni Dr. Njau akisisitiza kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dr. Laurent Mhembe (kulia) ,aliyewakilisha kituo cha afya cha Kambarage juu ya umuhimu wa kutunza vifaa hivyo kwa manufaa ya vijana
Zoezi la makabidhiano linaendelea
Miongoni mwa redio (Subwoofer systems)zilizotolewa na shirika la AGPAHI

Dr. Njau akikabidhi Redio (Subwoofer systems) kwa kwa Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa (katikati) na kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dr. Laurent Mhembe (kulia) aliyewakilisha kituo cha afya cha Kambarage

Dr. Njau akikabidhi vifaa vya michezo kwa Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. John Majigwa (katikati) na kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dr. Laurent Mhembe (kulia) aliyewakilisha kituo cha afya cha Kambarage

Kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dr. Laurent Mhembe (kulia) aliyewakilisha kituo cha afya cha Kambarage akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo kwa ajili ya vijana ambapo aliwataka vijana hao kutumia vyema vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa huku akiliomba shirika hilo kuendelea kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Shinyanga katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA