MHADHIRI UDOM AUTAKA URAIS NA UBUNGE. ADAIWA KUAFANYA KAMPENI MCHANA KWEUPE


Na, Mwandishi wetu Fichuzi news blog.

📌Akinzana na kauli ya Dkt. Nchimbi, atoa vitisho kwa wananchi.


Dr Phelemon Sengati aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Magu na baadae kutumbuliwa kwa kuzuia Dengu za wakulima Shinyanga, aibukia Ngara na kuanza kufanya kampeni Za Ubunge kabla ya wakati huku akijinasibu kuja kuwa Waziri na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Mnamo 14/5/2025 Majira ya saa nne Za asubuhi, Mhadhiri huyo alialika Mabalozi na Viongozi wengine wa Matawi, Kata ya Mugoma kwenye Tawi la Shanga, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera na alifanya kampeni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake Jimboni humo ambazo amekuwa akizifanya kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua na Ngazi Za Chama husika. 


Mhadhiri huyu amekuwa akituhumiwa kutumia vibaya majina ya Viongozi wakubwa kwenye Chama na Serikali wakati anapokuwa akifanya kampeni zake Kwa kuwa nijambo alilolizoea alisikika kwenye clip ya video akitaja viongozi Mbali mbali akiwemo rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na kuwatisha wajumbe na Watu kuwa atakuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Aidha wakati akinadi Sera zake eneo la Muruvyagira kata ya Mugoma, alianza kusema Maneno yaliyoibua hisia Za wajumbe ikiwemo kusema yeye ni Rais Ajaye jambo lililozua taharuki kwa Wajumbe nakuanza kujibizana nao mpaka walipo anza kutumia Simu zao kumurekodi ‘Amesena Mjumbe ambaye jina lake limehifadhiwa’.


Wakati wa Mahojiano na Mjumbe huyo amesema kuwa ‘tulishitushwa na Maneno ya Dr Sengati kuwa yeye ndiye Rais ajaye wa Tanzania huku tukijua kuwa Rais ajaye ni Dr SAMIA SULUHU HASSAN na si Mtu mwingine, Tuliogopa nakuhisi kuwa Dr. Sengati anaweza pengine kuwa na mpango mbaya dhidi ya viongozi wetu  ukizingatia kuwa alisema yeye anamtandao mkubwa sana Nchi hii. Amesema Mjumbe huyo ambaye jina limehifadhiwa. 


Miongoni mwa kauli alizotoa Dr. Sengati kwa wajumbe na chapisho alilolitoa kupitia Mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao wa Whatsapp anasema "Mimi nipo imara na mzima kabisa nyumbani kwangu keza na tarehe 28.6.2025 kama nipo hai nitachukua form ya kuomba ridhaa ya wanaNgara niwe Mbunge wa jimbo letu pendwa. Mungu ibariki Ngara yetu na Mungu ibariki Tanzania" Alisema dkt. Sengati




Hata hivyo kitendo cha Dr Sengati ni kinyume na Sheria na katiba ya ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) na kuonyesha kudharau na kupuuza kauli ya Katibu Mkuu CCM dkt. Emmanueli Nchimbi aliyotoa onyo la kupiga kampeni la waondoa majimboni wabunge waliopo madarakani ambayo alisema kufanya hivyo ni kupuuza katiba na kanuni ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM. 


"Tunapoelekea katika uchaguzi  kupuuza katiba na kanuni ni kosa kubwa la kimaadili ndani ya chama chetu, wapo watu ambao wameanza kampeni za kutaka kuwaondoa majimboni wabunge waliopo madarakani katika maeneo yao na kampeni chafu, natumia nafasi hii kuwasihi wana CCM kuhakikisha tunatumia mwaka huu kupata viongozi safi na bora, tuchague viongozi wanaochagulika." Alisema dkt. Nchimbi



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA