Hizi ni sauti za Team ya Dr Sengati ikigawa TZS 2,000 kwa wajumbe wa Mubuhenge kata ya Mugoma Wilayani Ngara Jana. Mda mchache baada ya kutoka Tawi la Muruvyagira kata hiyo hiyo ya Mugoma.
👇👇
Ikumbukwe kuwa ni baada ya Mnamo 14/5/2025 Majira ya saa nne Za asubuhi, Mhadhiri huyo kualika Mabalozi na Viongozi wengine wa Matawi, Kata ya Mugoma kwenye Tawi la Shanga, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera na alifanya kampeni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake Jimboni humo ambazo amekuwa akizifanya kwa muda mrefu bila kuchukuliwa hatua na Ngazi Za Chama husika.
Huku akikabiliwa na tuhuma nzito za kutumia vibaya majina ya Viongozi wakubwa kwenye Chama na Serikali wakati anapokuwa akifanya kampeni zake Kwa kuwa ni jambo alilolizoea alisikika kwenye clip ya video akitaja viongozi Mbali mbali akiwemo rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na kuwatisha wajumbe na Watu kuwa atakuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post a Comment