WIZARA YA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA YAOMBA BIL. 119

 Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi Bilioni 119 ikiwa ni makadirio ya Mapato na Matumizi Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.

Ni kufuatia hotuba yaWaziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi 119,017,998,000 na kuwa kati ya fedha hizo, shilingi 75,451,494,000 ni matumizi ya kawaida ambapo shilingi 63,086,267,000 ni mishahara na shilingi 12,365,227,000 ni matumizi mengineyo.

Dkt. Kijaji amesema shilingi 43,566,504,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo shilingi 30,346,819,000 ni fedha za ndani na shilingi 13,219,685,000 ni fedha za nje.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA