KAMISHNA JENERALI ARETAS LYIMO AFANYA ZIARA KWENYE KLINIKI YA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU (METHADONE) ARUSHA


Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo leo Juni 27, 2023 ametembelea Kliniki ya Tiba Saidizi kwa waraibu (Methadone) iliopo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru na kuangalia huduma inayoendelea kutolewa kwenye kliniki hiyo.

Aidha, ameupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuendelea kutoa huduma za tiba kwa Waraibu na kueleza kuwa Maamlaka  itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwenye kliniki hiyo 

Naye, Mganga Mfawidhi wa Mount Meru Dkt. Alex Ernest ameshukuru Mamlaka kwa kuendelea kutoa misaada kwenye kliniki hiyo kuanzia ujenzi wa jengo la kliniki, samani pamoja na vifaa tiba vinavyorahisisha uendeshaji wa huduma hiyo.


 Ameongeza kuwa hosptali hiyo imefanikiwa kutenga eneo la mafunzo ya kilimo cha mbogamboga ili  kuwasaidia waraibu kupata ujuzi na kutumia kama fursa ya kujipatia kipato.


Akisoma risala fupi mbele Kamishna Jenerali Mkuu wa kitengo cha Methadone Dkt. Salum Said ameeleza kuwa  Kliniki ya tiba saidizi ya waraibu (Methadone) ni kliniki inayotoa dawa ya Methadone kwa waraibu wa dawa za kulevya kwa Mikoa mitatu Arusha, Kilimanjaro na Manyara na kwa kipindi cha miaka miwili tangu ianzishwe imehudumia waraibu wapatao 616, wanaume wakiwa ni asilimia 82 na wanawake asilimia 18.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA