Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliotishwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani Mhe. Twaha Mpembenwe uliokuwa na lengo na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika Mkutano huo uliofanyika Julai 15,2023 ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Cde Abdulrahman Kinana, Mhe. Mayenga maarufu Dada Mkubwa alimshika mkono Mbunge wa Kibiti Mhe. Mpembenwe kwa kumchangia mabati 150 kwa ajili ya kukamilisha upauaji wa madarasa katika shule ya Sekondari ya Msala.
Post a Comment