WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WATEMBELEA BANDARI ZA ZIWA VICTORIA NA BANDARI YA NCHI KAVU ISAKA

Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wametembelea Bandari zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ajili ya kujionea na kujifunza namna zinavyofanya kazi. 

Bandari walizotembelea ni pamoja na Bandari ya Nchi Kavu ya Isaka wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga pamoja na Bandari za Ziwa Victoria (Kusini na Kaskazini)

Wakitembelea bandari hizo Agosti 30,2023,  waandishi wa habari wamejionea namna Serikali inavyowekeza kwa kufanya maboresho makubwa kwenye Bandari hizo na kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Meneja Bandari za Ziwa Victoria Frednand Nyathi, amesema katika maboresho ya Bandari tatu za Mwanza Kaskazini, Kemondo na Bukoba, Serikali imetenga kiasi cha fedha Sh. bilioni 60 kwa ajili ya kuzikarabati.

Amesema maboresho hayo yataongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Bandari pamoja na kuongeza mapato na kukuza uchumi wa nchi.

Afisa Bandari ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Abel Mshana amesema Bandari hiyo imekuwa ikiwahudumia wateja wa ndani na nje ya nchi na imekuwa ikirahisisha utendaji wa bandari na imekuwa ikihudumia nchi tano kusafirisha mizigo ikiwemo Rwanda,Burundi,Uganda, Sudani Kusini na DRC.

 Amewashauri wafanyabiashara na wadau kutumia bandari hiyo ili kupunguza gharama na muda wa kusafirisha mizigo.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC) iliyoandaa ziara hiyo, Greyson Kakuru amesema katika ziara hiyo wamejifunza mambo mengi ya uwekezaji wa Bandari ambao ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hapa nchini ikiwemo maboresho makubwa ya bandari.

Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Ferdinand Nyathi akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea Bandari za Ziwa Victoria

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza wakati waandidhi wa habari walipotembelea Bandari za Ziwa Victoria
Waandishi wa habari wakitembelea Bandari za Ziwa Victoria

Afisa Bandari ya Nchi Kavu Isaka mkoa wa Shinyanga Abel Mshang'a akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea bandari ya Nchi Kavu Isaka

Waandishi wa habari wakitembelea bandari ya Nchi Kavu Isaka

Waandishi wa habari wakipiga picha ya kumbukumbu katika bandari ya Nchi Kavu Isaka

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA