Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 23 Oktoba, 2023 ameshiriki vikao vya Makundi ya Mabara yanayounda Umoja huo katika Ofisi za Bunge la Angola zilizopo Jijini Luanda kwa lengo la kujinadi na kueleza sababu za yeye kugombea nafasi hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewaeleza Wajumbe wa Makundi hayo kuwa endapo watamchagua katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 atahakikisha anasimamia misingi ya Umoja huo kwa kuongeza Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi.
Post a Comment