YANGA WAFANYA MAUAJI KWA MKAPA!! WAIDUNGUA SIMBA SC 5-1

 


Dakika 90 za Mchezo wa Kariakoo Dabi Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam zimemalizika kwa shangwe kubwa kwa Yanga SC na kilio kizito kwa Simba SC!!! Yanga SC wameichakaza Simba SC Bao 5 - 1.

Kipindi cha pili Yanga walionyesha wanahitaji ushindi na kufunga mabao kupitia kwa Maxi Nzengeli ambaye alifunga mawili dakika ya 64, 77, Aziz KI dakika ya 73, Pacome bao la tano dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti.

Dakika 45 za mwanzo ubao umesoma Simba 1-1 Yanga.

Bao la Yanga lilifungwa dakika ya tatu na Kennedy Musonda na bao la Simba limefungwa na Kibu Dennis dakika ya 8.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA