MGODI WA MWADUI WAPANDIKIZA VIFARANGA VYA SAMAKI BWAWA LA MWANG'HOLO


Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akizindua zoezi la upandikizaji Vifaranga vya Samaki katika Bwawa Jipya la Mwang'olo.
Muonekano wa Vifaranga vya Samaki aina ya Sato.

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MGODI wa uchimbaji Madini ya Almasi (WDL) uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, umepandikiza vifaranga vya Samaki aina ya Sato katika Bwawa Jipya la Mwang'holo, ili kuinua kipato cha wananchi pamoja na kupata kitoweo.

Zoezi hilo la upandikizaji vifaranga vya Samaki limefanyika leo Desemba 8,2023 kwa kuzinduliwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo, akizungumza katika zoezi hilo, amesema wametekeleza agizo la Serikali la kurudisha kila kitu ambacho kiliharibika baada ya kupasuka kwa Bwawa la Majitope la Mgodi huo Novemba mwaka 2022.

Amesema zoezi la ulipwaji fidia kwa Waathirika, limemalizika na sasa wanachofanya ni kurudishia Mazingira ikiwamo upandaji miti, na kupandikiza vifaranga vya Samaki katika Bwawa Jipya, ili wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida ikiwamo uvuvi wa Samaki.

"Baada ya kupasuka kwa bwawa la kuhifadhia Majitope, liliathiri Bwawa ambalo wananchi walikuwa wakilitumia kufanya shughuli za uvuvi wa Samaki," amesema Mihayo.

"Baada ya kujenga Bwawa hili Jipya katika Kijiji cha Mwang'olo,tumetekeleza Maagizo ya Serikali na leo tumekuja kupandikiza vifaranga vya Samaki 5,000 aina ya Sato ili wananchi waendelee na shughuli zao za uvuvi kama zamani," ameongeza Mihayo.
Aidha, amesema katika zoezi la upandaji miti ili kutunza Mazingira katika vijiji vyote vinavyozunguka Mgodi huo kwamba hadi sasa wameshapanda Miti 10,000 na zoezi hilo ni endelevu.

Naye Afisa Uvuvi wilaya ya Kishapu Moses Ng'winza, ametoa wito kwa wananchi wasubiri hadi miezi Sita Samaki hao watakuwa tayari wamekuwa wakubwa, pamoja na kusubiri maelekezo kutoka Serikalini na kupewa elimu ndipo waanze shughuli za uvuvi.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed, ameupongeza Mgodi huo wa Mwadui kwa kutekeleza Maagizo ya Serikali, na leo wamezindua zoezi la upandikizaji vifaranga vya Samaki.

Amewataka wananchi kulitunza bwawa hilo, na kila mmoja awe mlinzi wa mwezake pamoja na kuacha kulima Kando ya bwawa ili Samaki hao waje kuwa msaada mkubwa kwao kiuchumi na kupata kitoweo.

Nao baadhi ya wananchi hao akiwamo Mvuvi Laurent Fabiani, amesema wanaushukuru Mgodi huo kwa kupandikiza vifaranga vya Samaki katika bwawa jipya, ili warudi katika shughuli zao za uvuvi na kujiongezea kipato, ambapo kwa sasa anaendelea na Kilimo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akizungumza kwenye zoezi la upandikizaji Vifaranga vya Samaki katika Bwawa la Mwang'olo kutoka Mgodi wa Almasi Mwadui.
Meneja Mahusiani Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akizunguma kwenye zoezi hilo la upandikizaji Vifaranga vya Samaki.
Afisa Uvuvi wilayani Kishapu Moses Ng'winza akizungumza kwenye zoezi hilo la upandikizaji Vifaranga vya Samaki.
Mwananchi Mussa Masanja akipongeza zoezi hilo la upandikizaji Vifaranga vya Samaki.
Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akizindua zoezi la upandikizaji Vifaranga vya Samaki katika Bwawa Jipya la Mwang'olo.
Afisa Uvuvi wilayani Kishapu Moses Ng'winza akiweka Samaki katika Bwawa.
Bwawa la Mwang'olo.
Wananchi wakishuhudia upandikizaji wa Vifaranga vya Samaki.
Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akipanda Mti katika Nyumba za Wathirika wa Bwawa la Majitope.
Muonekano wa nyumba za Waathirika wa Bwawa la Majitope ambalo wamejengewa na Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa nyumba za Waathirika wa Bwawa la Majitope ambalo wamejengewa na Mgodi wa Almasi Mwadui.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA