Serikali imejipanga kuja na mchakato wa mabadiliko ya uwekezaji katika sekta ya kilimo wenye lengo la kujenga uchumi shirikishi ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza wakulima na kuwapa pembejeo kwani mkulima mdogo ndiyo wazalishaji wakuu katika sekta hiyo.
Hayo yamwesemwa leo na Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashekatika mkutano na wawekezaji wa ndani, uliondaliwa na wizara hiyo leo Disemba 18, 2023 Jijini Dar es salaam, mkutano uliohudhuriwa na Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo uliokuwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha uwekezaji katika sekta ya Kilimo.
Waziri Bashe amesema kuwa bajeti mwaka 2023-2024 ya Wizara ya kilimo inakaribia Trilioni 1.5 jambo ambalo linaakisi uwekezaji unaofanywa na Serikali kwa kufikia malengo ya kujenga uchumi shirikishi ili kuondokana na umasikini, kuwaendeleza wakulima wadogo kwa kuwapa mbinu za kuongeza uzalishaji na kuwapa pembejeo kwani mkulima mdogo ndiyo wazalishaji wakuu katika sekta ya kilimo.
"Ninaahidi kuwekeza nguvu katika ushirikishwaji wa sekta binafsi ili kupunguza gharama kwa serikali kwa kuwaunga mkono wazalishaji wa mbolea, mbegu, pamoja na viwatilifu wanaofanya shughuli zao ndani ya Nchi sambamba na kupunguza kiwango cha uagizwaji wa unga wa ngano, sukari pamoja na mafuta ya kula kwa kuhimiza wawekezaji kuwekeza zaidi katika kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali" Alisema Waziri Bashe
Naye Waziri wa Mipango na Uwekezaji Mhe.Prof. Kitila Mkumbo amewahakikishia wawekezaji hao kuwa serikali kupitia wizara ya Kilimo imejipanga kuwekeza katika nyanja za Teknolojia, Fedha na Mipango ili kuhakikisha kilimo kinazidi kuwa na tija kwani kilimo ni biashara pamoja na kuwapa uhuru wawekezaji kufanya biashara ya mazao.
“Leo kama ukijiuliza suala kubwa hapa ni uhuru wa kufanya biashara, Nchi zetu za Afrika ikiwemo Tanzania suala la wafanyabiashara ni changamoto kubwa na ninafurahi kwamba viongozi wenzangu, watumishi wa Umma na Serikali tumeungana na kulifanyia kazi hili kwa msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo mtatusikia na kutuona sana tukiongelea kuhusu hili swala.” Alisema Mkumbo.
Post a Comment