WANASIASA CHIPUKIZI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KWA TAIFA

Na, Mwandishi wetu - Dodoma.

Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi zimehimizwa kuwa na umoja na kuheshimiana wao kwa wao ili kujenga taifa lenye tija kwasasa na vizazi vijavyo.

Hayo yamesemwa Leo na Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mhe. Jokate Urban Mwegelo wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu wa 9 wa Chipukizi wa CCM Taifa ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kwani ndiyo nguvu kazi ya Taifa.

Ameeleza madhara ya kuwepo kwa misuguano baina yao ikiwa ni pamoja na kusababisha utengano hali itakayopelekea dhamira ya ujenzi wa Taifa kushindwa kutekelezwa kikamilifu.

“Bado mnaendelea na safari ndo mnachipukia kiumri, kimazingira, uzoefu na kiutendaji Bado mna nafasi ya kuweka alama njema kwa nafasi yenu ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kutimiza Malengo na ndoto zenu.” Amesema Jokate

“Ni wajibu kuhakikisha tunaendana katika chama, kuyaenzi ambayo wazee wetu wameyafanya kwa kumsaidia rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga kila hali inayoweza kuleta hali ya uvunjifu wa amani na utulivu” Amesema Jokate

Amehitimisha Hotuba yake kwa kuwataka chipukizi hao kuendelea kujifunza katika nyanja mbalimbali kwani wao ni hazina na tunu muhimu kwa taifa.

“Tunapaswa kutambua sisi ni akiba inatupasa kuendelea kujifunza vyema katika nyanja zote ikiwemo kisiasa, kiuchumi na kijamii, chipukizi ishikeni sana elimu” Amesema Jokate

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA