Na, Mwandishi Wetu - Dodoma
Mapema Leo Bunge la Tanzania limeanza rasmi vikao vyake Jijini Dodoma ambapo Vikao hivyo vinatarajiwa kudumu kwa muda wa wiki tatu kwa ajili ya kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na wadau mbalimbali katika miswada mitatu.
Bunge likisikiliza Miswada iliyowasilishwa bungeni leo Januari 30, 2024 Bungeni Jijini Dodoma. |
Miswada hiyo iliyowasilishwa bungeni hapo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani wa Mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023 na, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa mwaka 2023 hii ikiwa ni baada ya kuwasilishwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ambapo, kwa muda wa siku nne mfululizo, kamati ilipokea maoni kutoka kwa zaidi ya taasisi elfu moja na inatajadiliwa bungeni hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenister Mhagama na Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Joseph Mhagama wameiwasilisha bungeni hapo ambapo pamoja na mambo mengine Mwenyekiti huyo amebainisha maoni yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kutaka wakurugenzi wa halmashauri kuondolewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi.