NDOTO YA MWAMBA ERRIKSON INAPOTIMIA YA KUPAMBANIA UHAI WAKE




Kocha Sven Goran Eriksson ambaye yupo kwenye nyakati za mwisho za maisha yake, Madaktari walimpima na kugundua ana saratani ya kongosho, hana muda wa kuzidi mwaka kwenye uhai wake, hayo ni majibu tangu mwezi Januari.


Wakati anafanyiwa Interview akatoa ombi lake kabla ya kifo chake (dying wish) akamwambia Mwandishi ndoto yake kabla ya kifo ni kusimama Anfield kama Kocha na kuifundisha Liverpool, baada ya hilo atakuwa radhi kuondoka duniani wakati ndoto yake imetimia. 



Liverpool walipopata taarifa hizo Kocha Jurgen Klopp akamkaribisha Errikson wakati wowote mpaka kufikia mwishoni mwa msimu, lakini ndoto hii imetimizwa wiki iliyopita ambapo Wakongwe wa Liverpool walicheza mechi ya hisani dhidi ya Ajax ya Uholanzi, yeye akapewa nafasi ya kuwa Kocha wa Liverpool. 



Alipokewa kwa shangwe nyingi sana na amefurahi kutimiza ndoto yake, wakati wowote mwaka huu ataondoka zake duniani lakini amesema wazi anaenda kupumzika wakati ndoto yake imetimia, kumbuka Madaktari wamempa makadirio ya kuwa hawezi kuvuka huu mwaka.

 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA