Mke wa mzee Gachuma afariki.
"Napenda kuwapa taarifa wanachama wote na makada wote wa CCM, tumepokea taarifa ya Msiba wa Mke wa MNEC wetu Mzee Mwita Gachuma amefariki na taarifa kamili za Msiba tutapeana kadri familia itakavyokuwa inatuletea."
Taarifa ya msiba huo imethibitishwa na Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mara Ndg, Simon Rubugu kilichotokea leo Jumamosi tarehe 23 Machi, 2024.
"Wote kwa pamoja tuungane kumfariji mzee wetu Gachuma na Binti yake Noela katika kipindi hiki kigumu."
Fichuzi Media inatoa pole kwa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Ndugu, Jamaa na Marafiki walioguswa na msiba huo.
Post a Comment