WASTAAFU NA MIKOPO YA SERIKALI CHANZO CHA KUZOROTA KWA MFUKO WA BIMA YA AFYA

 

"Mfuko wa bima ya afya imekuwa ikipata hasara kwa miaka mitano iliyopita mwaka wa fedha 2022/23 hasara ilikuwa Tsh. Bilioni 156.77 ikipungua kutoka Bilioni 205.95 kwa mwaka 2021/2022, Aidha michango ya wanachama imeongezeka kwa  14.6% na matumizi yameongezeka kwa 10% Hali hii inaonyesha uwepo wa jitihada za kuboresha Hali ya mfuko hata hivyo Kuna mambo yanaweza kuathiri uhai wa muda mrefu wa mfuko wa huduma ya afya  ikiwemo mikopo ya serikali ambayo haijalipwa na Changamoto nyingine ni Wastaafu kunufaika bila kuchangia, Wastaafu na wenza wao wanapata huduma bila kuchangia na hii inagarimu mfuko Shilingi Bilioni 84.70 kwa mwaka" Alisema Charles kichere

Hayo yamebainishwa na mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Charles kichere Leo Machi 28, 2024 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma wakati wa kukabidhi ripoti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya mwaka 2022/2023.

Awali kabla ya tukio hilo Rais Samia amepokea taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU ya mwaka 2022/ 2023.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA