NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kulazimishwa sare na Mamelodi Sundowns 0-0.
Katika
mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es
Salaam, Mamelodi waliweza kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza
ambapo walitawala kwa asilimia 73% kwa 23% licha ya Yanga Sc kuwa na
mashuti matatu yaliyolenga lango huku Mamelodi wakiwa wamepiga moja tu.
Kipindi
cha pili Yanga walibadilika na kuonesha hali ya kulitaka bao la
kuongoza bila mafanikio licha ya kupata nafasi za wazi nyingi.
Sifa
za kipekee zimuendee mlinda mlango wa kimataifa wa Afrika Kusini,
Ronwel Williams ambaye aliokoa hatari nyingi ambazo zilitengenezwa na
Yanga Sc.
Post a Comment