KATAMBI AKABIDHI MAGARI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA

 


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini amekabidhi gari moja la kubeba Wagonjwa (Ambulance) gari la Utawala la shughuli za usimamizi Shirikishi na gari aina ya TATA kwa ajili ya kubeba Watumishi wa Afya kutoka majumbani na kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Ijumaa Mei 24,2024 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mhe. Katambi amesema lengo la magari hayo ni kuboresha huduma za afya ikiwa ni dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha huduma za afya nchini.

Katambi amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kutoa fedha nyingi na kuboresha huduma za afya hapa nchini.


“Ndani ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Utawala wake ndani ya kipindi kifupi ameleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya likiwemo Jimbo la Shinyanga Mjini. Kwenye sekta ya afya tumefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 100 mkoani Shinyanga",amesema Katambi.
Katika hatua nyingine Katambi amesema serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo katika Hospitali ikiwemo upungufu wa miundombinu ya majengo, Watumishi, ubovu wa barabara.

"Tutaongeza Ambulance nyingine katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, tutaijenga hii barabara pia, lazima tuweke lami hapa wagonjwa wasipate usumbufu. Tutaendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo”,amesisitiza Katambi.

“Leo ninakabidhi magari haya matatu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, ni jambo jema sana katika kuboresha huduma za afya na kuwajali watumishi kwa kuwapatia usafiri", ameongeza Katambi.
Mhe. Patrobas Katambi

Kwa upande, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro amesema mambo ambayo anayafanya Katambi Jimboni kwake ni maajabu, na ni bahati ya pekee waliyonayo Wanashinyanga kuwa na Mbunge mpenda Maendeleo na hana kelele zaidi ya kuonesha vitendo.

Akitoa taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kuleta watumishi.


“Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ilipata mgao wa magari mawili (gari la wagonjwa na gari la shughuli za utawala ambalo linafanya kazi za usimamizi shirikishi. Pia kupitia makusanyo ya ndani Hospitali imeweza kununua gari la watumishi aina ya basi (Tata). Mgao huu wa magari ni matokeo ya utekelezaji wa miradi ya Afya kwenye Kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko – 19 kwa kutumia mkopo wa masharti nafuu shirika la Fedha Duniani (IMF)”,ameeleza Dkt. John.
“Hospitali inatoa shukrani za dhati kwa mhe. Rais Samia na wewe mwenyewe Mhe. Mbunge kwa namna ulivyosaidia katika upatikanaji wa magari haya na namna ambavyo umeendelea kufuatilia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya majengo kama vile jengo la Mama na Mtoto, Mochwari, Incinilato, Jengo la ufuaji na maabara”,amesema Dkt. John.

Amezitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na uchache wa miundombinu ya majengo katika hospitali hiyo ili kukidhi kutoa huduma zote katika hospitali mpya, upungufu wa watumishi 225 (47%).

Dkt. John amesema changamoto nyingine ni kuharibika kwa barabara ambayo haijajengwa kwa kiwango cha lami kutoka Mjini Shinyanga hadi ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga hivyo kuleta usumbufu kwa wagonjwa hususani wagonjwa mahututi na waliovunjika mifupa hivyo kuiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami na upatikanaji wa Ambulance nyingine.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI





Muonekano wa magari yaliyokabidhiwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Muonekano wa magari yaliyokabidhiwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga

Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu  akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA