MASHINDANO YA UMISSETA YAANZA KUTIMUA VUMBI TABORA



Ikiwa leo Mashindano ya 28 ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yakifunguliwa, tayari mikoa kadhaa imeanza vizuri safari ya kuwania ubingwa wa michezo hiyo inayofanyika mkoani Tabora.

Katika michezo ya awali hatua ya makundi kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana, wenyeji Tabora wameachapa Kigoma pointi 48-24, Dodoma ikilala kwa Mbeya kwa pointi 51-29.

Kwenye mchezo wa mpira wa wavu wasichana Katavi imefungwa na majirani zao Rukwa kwa seti 0-3, Manyara imeichapa Dodoma kwa seti 3-0 wakati kwa upande wa wavulana Dar es Salaam wameichapa Arusha kwa seti 3-0 huku Mara ikiishia Mtwara kwa seti 2-1.


Katika mchezo wa mpira wa mikono wasichana, Manyara imeishinda Njombe mabao 11-10, Pwani ikilala dhidi ya Kagera kwa mabao 24-12 na Tabora ikiwafunga Kilimanjaro kwa mabao 32-18.

Kundi B Shinyanga ilikuwa hoi kwa Mbeya kwa mabao 23-11 na Dar es Salaam ikiishinda Katavi mabao 18-12 huku kwa kindi V Tanga ikiichapa Mwanza kwa mabao 23-12 na Singida ikiishinda Rukwa mabao 13-12 wakati kundi D Mara ikiishinda Kigoma mabao 22-16 na Iringa ikiishinda Lindi kws mabao 12-8.

Katika mchezo wa soka wavulana, Unguja imetoka suluu na Kilimanjaro na Morogoro ikiibuka kidedea kwa mabao 3-1 dhidi ya Iringa.
Pia Singida imeichapa Arusha kwa mabao 2-1, Dodoma ikichoshana nguvu na Mwanza baada ya kutoka suluu na Geita ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi Mara na Mtwara ikiwachapa kwa bao 2-0.




 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA