OR-TAMISEMI
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde
amewataka watendaji wa Hamshauri nchini kushughulikia uhamisho wa walimu
na watumishi wengine kwa kutumia mfumo uliowekwa ili kuondoa sitofahamu
zinazojitokeza.
Dkt.
Msonde ametoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi cha majumuisho ya ziara
ya katika mkoa wa Tabora kilichowakutanisha walimu,walimu wakuu,wakuu wa
shule,Maofisa Elimu na wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa huo
kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mihayo Manispaa ya
Tabora.
“Siku
zote kuwa makini kuona kwenye mfumo tunapitisha nini kwasababu watu
wameomba uhamisho ni lazima tuwapitishie ili mwenye mamlaka ya
kuidhinisha uhamisho akiona haitahili yeye atakataa lakini sisi
tuwapitishie kulingana na maombi yao, ” amesema
Dkt.
Msonde amesisitiza kuwa endapo mkurugenzi atakuwa amebanwa na shughuli
zingine na kushindwa kuingia kwenye mfumo anapaswa kukasimu mamlaka kwa
mtu mwingine ili kuhakikisha maombi hayakai kwa muda mrefu na kuwaacha
watumishi wakilalamika.
Akizungumza
kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora, Grace
Quintine ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
ameahidi kufanyia kazi maelekezo hayo na kuyasimamia ili kuwe na
ufanisi katika sekta ya Elimu katika mkoani humo.
Post a Comment