Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lina mshikilia mtuhumiwa mmoja alie jifanya mtumishi wa serikali Afisa biashara katika Halimashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 05,2024 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Davidi Mutasya amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo aliyejifanya mtumishi wa serikali kwa lengo la kuwaibia wananchi kupitia cheo hicho.
Sambamba na hayo Mutasya amebainisha kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa 51 na kuhukumiwa vifungo mbalimbali.
Amesema watuhumiwa wawili walihukumiwa miaka 20 jela kwa kosa la kupatikana na nyara za serikali, mtuhumiwa mmoja miaka mitano jela kwa kosa la wizi wa Mifugo alikadhalika watuhumiwa wengine kwa makosa yanayo landana na hayo.
Amebainisha kuwa kwa upande wa usalama barabarani Jeshi la hilo limezuia ajali kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazo endelea ikiwemo utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara.
Amesema katika kuimarisha usalama barabarani jeshi hilo limefanikiwa kuongeza nguvu na umakini katika ukaguzi wa Madereva wakati wa kiendesha vyombo vya moto na kufanikwa kukamata jumla ya makosa 2057 ambayo yalikuwa yanachangia ongezeko la ajali barabarani.
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lina toa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo viovu vya kihalifu na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Jeshi hilo liweze kuchukua hatua za kisheria na kuimarisha ulinzi na usalama katika jaamii.
Post a Comment