TRA YAHAMASISHA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI KWA WAKATI

Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi akizungumza leo Jumatano Septemba 25,2024  katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni, kero na changamoto za wafanyabiashara.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewahimiza Wafanyabiashara walipe kodi stahiki na kuwasilisha marejesho ya kodi kwa wakati ili kuepuka adhabu na riba endapo watachelewa.

Wito huo umetoewa leo Jumatano Septemba 25,2024 na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni, kero na changamoto za wafanyabiashara.
“Ni wajibu wako kuzingatia tarehe za kulipa kodi stahiki bila nyongeza yoyote kwa wakati, unatakiwa kulipa kodi unayostahili wafanyabiashara, mna wajibu wa kuwasilisha marejesho ya kodi kwa wakati, kodi ikichelewa kulipwa ina riba. Tambua tarehe za kuwasilisha Return na lipa kodi kwa wakati, ukileta umechelewa kuna adhabu na riba”
,amesema Mrengi.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi akizungumza na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga

“Tunaendelea kukutana na wafanyabiashara na kuzungumza nao kwani tunataka wafanyabiashara wafanye kazi kwa amani na kuwe na Fairness katika ulipaji kodi. TRA imedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano baina yake na Wafanyabiashara nchini, mnapokumbana na changamoto msisite kufika TRA, njooni tuzungumze lengo ni kuhakikisha mnachangia maendeleo ya nchi yetu”,ameongeza Mrengi.

Katika hatua nyingine amesema TRA inaendelea kwenda kwenye maeneo wanakofanyia biashara walipa kodi ili kuwasogezea karibu huduma.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaja amewashukuru Wafanyabiashara mkoani Shinyanga kwa kuendelea kuwa walipa kodi wazuri.

Amewasihi wafanyabiashara pindi wanapokutana na changamoto wawasiliane na maafisa wa TRA ili kutatua kero zao na kuwaomba watumie siku ya Alhamisi kukutana na TRA

Naye Kaimu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Shinyanga Khatibu Mgeja ameishukuru TRA kwa kuendelea kutoa fursa ya kukutana na wafanyabiashara ili kutoa maoni huku akiwahamasisha wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kufika TRA kueleza kero na changamoto zao badala ya kukaa kimya.

Mbali na kuishukuru TRA kwa kuendelea kutoa elimu mara kwa mara wameomba kuwe Mfumo wa kufanya malipo na mawasiliano na TRA kwa njia ya mtandao na wapewe Namba ya malipo (Control number) ya kulipa mara moja kwa mwaka badala ya kulipa kwa awamu na kulazimika kwenda TRA mara kwa mara.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi akizungumza leo Jumatano Septemba 25,2024  katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni, kero na changamoto za wafanyabiashara. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaja akizungumza kwenye kikao cha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaja akizungumza kwenye kikao cha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Kaimu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Shinyanga Khatibu Mgeja akizungumza kwenye kikao cha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 

Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga 
Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga wakiwa ukumbini

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA