JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA USAFIRI WA ANGA TANZANIA LAWAKUTANISHA WANAWAKE VIONGOZI JIJINI DAR ES SALAAM

 


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Juma Pembe ( wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa nembo ya Jukwaa la Wanawake katika usafiri wa anga Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Jukwaa hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam. Wa pili ni kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi. Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCAA Bi. Mtumwa Ameir
Mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Wanawake katika usafiri wa anga Tanzania umefanyika kwa mara ya kwanza ukiwakutanisha wanawake viongozi katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini.


Ufunguzi wa Jukwaa hilo umefanyika jijini Dar es Salaam ulifanywa na Mhe. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Juma Pembe, ambapo ametoa pongezi kwa wanawake kwa juhudi wanazozifanya katika kujipambanua katika usafiri wa anga.

Katika hotuba yake, Mhe. Riziki amesisitiza umuhimu wa serikali kuhakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa katika sekta zote.

 Ameeleza kuwa kila mtu anapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yake, huku akitoa wito kwa wanawake kuwa na ujasiri na kujituma katika kufanikisha ndoto zao.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, ametambua mchango muhimu wa wanawake viongozi katika jukwaa hilo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.

Bi. Maria Memba, ambaye ni mwanzilishi wa Jukwaa hilo na pia Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TCAA, ameongeza kuwa huu ni mwanzo tu wa safari ndefu ya kuwawezesha wanawake katika sekta ya usafiri wa anga.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuhamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi na maamuzi kwenye sekta hiyo. Hivyo, jukwaa hili linalenga kuleta mabadiliko chanya na kuhakikisha uwakilishi sawa wa wanawake katika usafiri wa anga Tanzania.

Jukwaa hili lilizinduliwa rasmi mwaka 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Juma Pembe, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCAA Bi. Mtumwa Ameir, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Katika Usafiri wa Anga Tanzania Maria Makalla Memba pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Prof. Neema Mori wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa nembo ya Jukwaa la Wanawake katika usafiri wa anga Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Jukwaa hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akizungumza kuhusu namna viongozi hao wanawake wanavyoweza kuibadilisha sekta ya usafiri wa anga wakati wa mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Wanawake Katika Usafiri wa Anga Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCAA Bi. Mtumwa Ameir akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma wakati wa Mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Wanawake katika usafiri wa anga Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akizungumzia namna Mamlaka hiyo inavyoshirikiana na Jukwaa la Wanawake Katika Usafiri wa Anga Tanzania wakati wa mkutano wa jukwaa hilo
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Katika Usafiri wa Anga Tanzania Maria Makalla Memba akizungumza kuhusu namna walivyoweza kuanzisha jukwsa hilo lililoweza kuwakutanisha wanawake viongozi katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wanawake viongozi katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini wakifuatilia mada katika Jukwaa la Wanawake Katika Usafiri wa Anga Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Juma Pembe(katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi(wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Prof. Neema Mori (wa kwanza kulia) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCAA Bi. Mtumwa Ameir (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Katika Usafiri wa Anga Tanzania Maria Makalla Memba(wa kwanza kushoto) waliokaa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali pamoja na wanawake viongozi katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini wakati wa Mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Wanawake katika usafiri wa anga Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA