NEEMA KWA WAKAZI WA NGARA, SERIKALI YA PELEKA MRADI MKUBWA WA MAJI, VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA

   

  

 Na, Mwandishi wetu.

Imekuwa ni neema kwa wananchi wa Kijiji cha Kigina Kata ya Ntobeye Wilayani Ngara Mkoani Kagera waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama wanatarajia kuondokana na Changamoto hiyo baada ya Serikali kupeleka mradi  mkubwa wa kuchimba kisima cha Maji.


Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe.Ndaisaba George Ruhoro wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji hicho cha kigina kata ya Ntobeye alipo fanya ziara ya kikazi na kumkabidhi mradi Mkandarasi atakayeutekeleza.


Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kutunza mradi huo ili uweze kuwahudumia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kumuasa mkandarasi anayetekeleza mradi huo kufanya kazi nzuri.


akipokea mradi huo Mkandarasi Bw.Joseph Buzubona  amemuahidi Mbunge huyo na wananchi kuwa mradi huo atautekeleza kwa wakati na kwaufanisi.

Sanjari na hayo ujio wa mradi huo umekuwa neema kubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo kwani vijana nao watapata nafasi ya kuchangamkia fursa za ujenzi wakati wa utekelezaji wa Mradi huo.


Nao wananchi wametoa shukrani zao kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumtua mama ndoo kichwani kwani wanalazimika kutembea umbali mrefu kufata maji.


Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Ntobeye wilayani Ngara Mhe.Sande Mkozi amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa kufanikisha mpango wa wananchi kupata maji safi.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA