VIJIJI VYOTE NEWALA VIMEFIKIWA NA UMEME - MHE. KAPINGA


-Asisitiza dhamira ya Serikali ni kupeleka umeme maeneo yote


Naibu Waziri Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Vijiji vyote 76 vya Jimbo la  ya Newala Vijijini Mkoa wa Mtwara vimefikiwa na huduma ya umeme kwa umbali wa kilometa 1. 


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la Mhe. Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala Vijijini aliyetaka kufahamu lini Serikali itaanza ujenzi wa nguzo za Kilomita 2 katika Vijiji ambavyo mradi wa  REA mzunguko wa Pili unatekelezwa.


"Kwa nyongeza ya umbali wa kilomita 2, REA kupitia Mkandarasi Central Electrical International Limited anaendelea na kazi na amefanikiwa kufikisha umeme kwenye vijiji 32 kati ya vijiji 76. Vijiji vilivyosalia vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni", Amesema Mhe. Kapinga


Akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Mhe. Abubakar Asenga aliyeuliza lini Serikali itaunganisha umeme katika Kitongoji cha Upendo, Tupendane, Ikwambi na Misheni katika mji wa Ifakara,  Mhe. Kapinga amesema vijiji hivyo vipo katika mradi wa vitongoji unaoendelea.


Amesema dhamira ya Serikali  ni kuhakikisha wanachi wote wanapata nishati ya umeme na hivi sasa upo mradi wa Vitongoji 15 kwa kila jimbo na kuongeza kuwa upo mradi mwingine wa Vitongoji unaotarajiwa kuanza.


Akijibu swali la Mbunge wa Mbarali, Mhe. Keneth Ndingo aliyetaka kujua lini Vitongoji vya Igula A, Igula B na Mngolongolo vitapata umeme, Mhe. Kapinga amesema vijiji hivyo vimeshafanyiwa mapitio na vipo katika mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15.


Mhe. Kapinga amesisitiza kuwa uunganishaji wa umeme utafanyika katika maeneo yote ya Vijiji.





Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA