WANANCHI 26,963,182 WAPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024


Zoezi  la uandikishaji wa wapiga kura lilifanyika kuanzia tarehe 11 mpaka 20 Oktoba, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha. Kati yao, wanawake walikuwa 16,045,559 na wanaume walikuwa 15,236,772. 


Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 na Kanuni ya 11 ya Tangazo la Serikali Na. 572 kulikuwa na muda wa wananchi kuweka pingamizi kwa wananchi waliojiandikisha. Baada ya kushughulikia pingamizi wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikuwa 31,255,303. 


Pingamizi za uandikishaji zilitokana na sababu mbalimbali ikiwemo wananchi kutokuwa wakazi wa maeneo husika na wengine kujiandikisha kwenye maeneo wanayofanya shughuli zao za kiuchumi badala ya maeneo yao ya makazi. Aidha, wananchi waliopiga kura siku ya tarehe 27 Novemba, 2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokuwa na sifa ya kupiga kura.





Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA