MBUNGE NDAISABA AUNGA MKONO AJENDA YA RAIS SAMIA, AMPA USHAURI HUU DKT. BITEKO

Na Mwandishi wetu - Fichuzi news blog.

Leo April 29, 2025 wabunge wameendelea kuchangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Nishati huku wakitoa pongezi na kuishauri serikali katika sekta hiyo ili wananchi waendelee kupata huduma bora ya umeme ikiwa ni pamoja na kuweka transfoma zenye KVA100 hadi 200 badala ya KVA 50, kupunguza kodi kwenye vifaa vya matumizi ya majumbani vya kielektroniki pamoja na kusambaza majiko ambayo yanauwezo wa kutumia umeme na gesi.

Ombi hilo limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro leo Aprili 29, 2025 wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati iliyowasilishwa bungeni hapo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Katika kukuza ajenda ya nishati safi ameshauri mitungi ya gesi inayosambazwa na REA iendane na majiko yanayokubali kupikia kwa kutumia umeme na gesi ikiwa ni pamoja na kuondoa makato (tozo) kwenye vifaa  vya kielektroniki kama vile majiko ya gesi, brenda, tv, n.k ili wananchi wa vijijini waweze kununua vifaa hivyo kwa garama nafuu.

"Ombi langu kwa serikali tunaomba muanze kutufungia transfoma zenye ukumbwa wa KVA 100 - 200 badala ya hizi zilizopo za KVA50 Hii itasaidia wananchi wengi kuunganishwa umeme na katika kuongeza matumizi ya umeme niwaombe Wizara kufanya mchakato wa mitungi ya gesi iende sambamba na majiko yanayokubali kutumia umeme na gesi, hii itasaidia endapo mwananchi akisubiri kwenda kununua mtungi wa gesi aweze kuunganisha jiko lake na kwa kutumia umeme uliopelekwa majumbani kwani kwasasa wananchi kwa kiasi kikubwa wanatumia umeme huo kwa matumizi ya mwanga, na viwanda", amesema Ndaisaba

"Naomba kujua TANESCO na REA wamejipangaje kurudisha huduma ya umeme ikitokea umekatika ama miundombinu imesumbua , nina vijiji vitano ambavyo Transfoma zimeungua na wananchi wanasubiria huduma ya umeme kwa muda mrefu ambavyo ni Mkalinz, Kititiza, Mkubu, Mumilamila, na Mganza nakuomba Mheshimiwa Waziri uje na suluhu ya ni lini wananchi wangu watapata huduma wakati utakaokuja kuhitimisha hoja",amesema Mbunge wa Ngara.

Aidha katika hotuba yake ametoa pongezi nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ajenda ya nishati safi kwani kwa kiasi kikubwa imeondoa matumizi ya vibatari katika maeneo mengi vijijini hasa katika jimbo la Ngara, pongezi hizo pia amezitoa kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Doto Biteko na wasaidizi wake kwa utendaji kazi uliotukuka.

Video hii hapa 👇👇



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA