BARRICK YAWEZESHA NA KUSHIRIKI KONGAMANO LA AIESEC LA KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI VYUO VIKUU ARUSHA

 

Wanafunzi wakigawiwa vipeperushi vyenye miongozo ya kuchangamkia fursa za ajira
Wanafunzi wakiwa ukumbini
Wanafunzi wakiwa ukumbini
Mmoja wa washiriki akiuliza swali
Wageni katika meza kuu wakifuatilia matukio
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo
**

Kampuni ya Barrick nchini kwa mara nyingine imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha, lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha (IAA).

Kupitia kongamano hilo, Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha wamepatiwa mbinu mbalimbali kutoka kwa wataalamu, za kuchangamkia fursa zinazojitokeza ikiwemo za ajira, kujiajiri pia jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea kutokea siku hadi siku yanayoathiri upatikanaji wa ajira.

Pia Wanafunzi wamewezeshwa kujua jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kujifunza, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Wanafunzi pia wamepata nafasi ya kujua shughuli zinazofanywa na kampuni ya Barrick na programu mbalimbali za kijamii zinazotekelezwa na migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa.

Wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo wamepata fursa ya kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira,ubunifu na jinsi ya kuendeleza vipaji vyao pia mchango wa kampuni katika kukuza uchumi wa kijamii nchini sambamba na kutekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Milenia.

Barrick imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu mbalimbali nchini kupata mafunzo ya vitendo katika katika migodi yake‘Field attachments’, sambamba na kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania wenye weredi wa taaluma mbalimbali katika migodi yake nchini pia imekuwa ikitekeleza programu za kuwainua vijana kiuchumi ili wasibaki nyuma.

Kongamano la AIESEC mwaka huu tayari limefanyika katika vyuo vikuu vilivyopo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma,Iringa na Zanzibar kwa udhamini wa Barrick kwa kushirikiana na wadau wengine.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA