
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata ya Iselamagazi, Wilaya ya Shinyanga, Frank Ronald Mulokozi , leo Juni 30, 2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kwa ajili ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi , jimbo lililokatwa kutoka Jimbo la Solwa.
Frank Mulokozi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mulo Clearing & Forwarding inayojihusisha na huduma za usafirishaji hapa nchini Tanzania.
Mulokozi amesema ameamua kujitokeza kwa nia ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Itwangi kwa moyo wa kizalendo, uzoefu wa kibiashara na kiu ya maendeleo ya kweli kwa wananchi.
Post a Comment