Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Kishoa amechukua fomu hiyo leo Juni 30, 2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida
Hatua hiyo ya Kishoa inakuja ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu alipotangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi.
Kishoa ni miongoni mwa Wabunge 19 wa Viti Maalum kupitia Chadema walioingia kwenye mgogoro na Chama chao, hali iliyosababisha kufutiwa uanachama, baada ya uongozi kueleza kuwa taratibu za kupata ubunge hazikuzingatia kanuni, na miongozo ya Chama hivyo Ubunge wao sio halali.
Kishoa anatajwa kuwa miongoni mwa wagombea wanaotarajiwa kuleta ushindani mkubwa katika kinyang’anyiro hicho, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja pamoja na nguvu ya ushawishi aliyokuwa nayo katika ulingo wa kisiasa.
إرسال تعليق