Na mwandishi wetu Malunde 1 Blog
Mzalendo Leonard Nduta Lukanya, kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Solwa katika uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025 kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Mzalendo halisi Ndugu Leonard Nduta Lukanya amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo leo Juni 29, 2025 katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga akiwa na nia kubwa ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika maendeleo ya kiuchumi, siasa, diplomasia na kijamii.
Ndugu Leonard amejitosa kwenye nafasi hiyo akiwa na dhamira kubwa katika masuala mbalimbali kwa maendeleo ya watu wa jimbo la Solwa.
Mosi, kuuwasha mwanga wa ukombozi kwa wana Solwa.
Pili, Kuliunganisha jimbo la Solwa na viunga vyake kama ilivyo ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Tatu, Kuimarisha miundombinu ya taasisi kwa jimbo la Solwa ambapo utakuwa ni mwendelezo kwani tayari serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza.
Nne, Kufanyakazi ya kuisema jamii kwa serikali yetu sikivu ili kuweza kushughulikia changamoto na masuala mbalimbali katika jimbo la Solwa.
Ikumbekwe kuwa Ndugu Leonard Nduta Lukanya Mzalendo na Mtia nia katika jimbo la Solwa alizaliwa katika kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza wilaya ya Shinyanga Vijijini.



إرسال تعليق