SERIKALI KUJA NA MPANGO KABAMBE YA KUSAMBAZA MICHE BORA YA PARACHCHI LAKI MOJA 2025/2026


Na, Mwandishi wetu - Fichuzi blog

Serikali imeeleza kuja na mpango mkakati wa kuzalisha na kusambaza bure Miche bora ya parachichi katika Wilaya ya Ngara ikiwa ni pamoja na kuupokea na kufanyia kazi ushauri wa Mbunge wa Jimbo hilo wa kuotesha miche hiyo ya parachichi sambamba na ilipo miche ya kahawa kwakuwa wana miundombinu bora na rafiki.

Hayo yemebainishwa na Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Davide Silinde wakati alipiokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro leo June 11,2025 bungeni Jijini Dodoma alilouliza kuwa "Je, Serikali ina mkakati gani wa kukuza kilimo cha parachichi Ngara."

Akijibu swali hilo Naibu Waziri amesema Mikakati inayotekelezwa katika Wilaya ya Ngara ni pamoja na kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa miche bora ya parachichi ambapo Taasisi ya Uthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ilitoa elimu ya uzalishaji wa miche, kutoa elimu ya kilimo bora na udhibiti wa visumbufu wa zao la parachichi na kuendelea kufungua masoko mapya ya parachichi nje ya nchi.

"Katika msimu wa 2023/2024 na 2024/2025, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilinunua na kusambaza bure miche bora ya parachichi 26,000 kwa wakulima. Pia, katika msimu wa 2025/2026 Wizara ya Kilimo itashirikiana na Halmashauri na sekta binafsi kuzalisha na kusambaza miche bora ya parachichi 100,000. Aidha, Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) imepanga kununua na kusambaza kiuatilifu maalum cha parachichi aina ya Copper Sulphate kwa lengo la kudhibiti magonjwa ya ukungu. Vilevile, majaribio ya mbolea maalum za zao la parachichi yanaendelea ili viwanda vya ndani viweze kuzalisha mbolea hiyo." Amesema Silinde

Hata hivyo kufuatia majibu hayo ya serikali Mbunge huyo akasimama kwa swali la nyongeza alilouliza kuwa "Kwakuwa kule Ngara tumeshaandaa vitalu vinne ambavyo vimepelekwa karibu na makazi ya wananchi kwaajili ya kuotesha miche ya kahawa na kwakuwa tayari tuna miundombinu ya kutosha inayo'sapoti' kuotesha miche ya kahawa huko vijijini, huoni kuna umuhimu wa hii miche ya Parachichi ikaoteshwa sambamba na ilipo miche ya kahawa ili iweze kuwafikia wananchi kwa uharaka na urahisi?" Ameuliza Mbunge Ruhoro

"Nimpongeze sana Mbunge Ndaisaba kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo lake na nimdhibitishie kuwa maoni yake tumeyapokea na tutayafanyia kazi" Amesema Naibu Waziri Silinde

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA