Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua 'Albino Mobile App' ambayo ni program ya simu janja itakayowezasha usajili na ukusanyaji wa taarifa za watu wenye Ualbino na wenye Ulemavu kwa njia ya kidigitali.

Aidha, amesema Mfumo wa Albino Mobile App ni sehemu ya Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD – MIS) utaongeza ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu kwenye huduna za kijamii na maendeleo.

Amesema hayo leo Juni 13, 2025 wakatu alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimiwho ya Siku ya Kimatqifa yw kukuza uelewa kuhusu Ualbino ambayo yamefanyika katika uwanja wa Mwanga Center, mkoani Kigoma.

Vile vile, amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu wenye Ualbino, Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi na Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD-MIS) katika ngazi ya Halmashauri.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema kuwa programu hiyo janja ya ' Albino Mobile App' itarahisisha na itahakikisha usahihi wa taaarifa za usajili wa watu wenye Ualbino katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mfumo huu utapunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa vifaa kwa ajili ya usajili, na pia kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi zinazosaidia Serikali kupanga na kutekeleza sera kwa ufanisi” amesema

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS), Godson Mollel amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendela kuwafanyia mambo makubwa watu wenye Albino nchini ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kuwezesha upatianaji wa mafuta kinga ambayo hugawiwa bure.