Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kKitaifa Ndg.Ismail Ali Ussi akizungumza baada ya kuona,kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 8,2025
Na Sumai Salum-Kishapu
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kupeleka miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kishapu, akieleza kuridhishwa na namna miradi hiyo inavyowanufaisha wananchi kwa uhalisia.
Ussi ametoa pongezi hizo leo Agosti 8, 2025, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Wilayani Kishapu Mkoani shinyanga ambapo amezindua, ameweka mawe ya msingi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema Kishapu imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na usimamizi mzuri wa miradi unaofanywa na viongozi wa Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Peter Masindi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bw. Emmanuel Johnson.
“Nimefurahishwa sana na kazi kubwa inayofanyika hapa Kishapu. Miradi yote niliyotembelea leo imetekelezwa kwa ubora, thamani ya fedha inaonekana na wananchi wameanza kunufaika moja kwa moja"ameongeza.
Aidha, amesisitiza kuwa usimamizi madhubuti kama huo unapaswa kuwa mfano kwa Halmashauri nyingine nchini, ili kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kikamilifu kwa maendeleo ya wananchi.
Katika ziara hiyo, Mwenge wa Uhuru umegusa miradi ya sekta ya maji,barabara,elimu,uwekezaji,afya na maendeleo ya vijana, ambapo miradi yote ilikidhi vigezo na kupita bila dosari.
Mwenge wa uhuru umekagua Kikundi cha Vijana Wachapakazi kilichopo Kata ya Songwa kinatekeleza mradi wa kilimo cha nyanya kwenye ekari tano kwa mkopo wa Shilingi 20,752,209/= kutoka asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri, ambapo tayari wameanza kurejesha kiasi cha Shilingi milioni 5, mradi huu unalenga kuinua uchumi wa wanakikundi na jamii inayowazunguka kwa kuwapatia ajira na kuongeza kipato chao kupitia kilimo cha mbogamboga.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter Msindi (kushoto) akikabidhiwa mwenge wa uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Manispaa Wakili Julius Mtatiro (Kulia) Agosti 8,2025 Katika Uwanja wa Kijiji cha Seseko Kata ya Songwa Wilayani Kishapu
Mwenge huo pia umezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa vyumba saba vya madarasa na matundu nane ya vyoo katika shule mpya ya sekondari ya Masagala kwa gharama ya Shilingi 196,400,000.
Lengo la mradi ni kuwasogezea wananchi wa kijiji cha Masagala huduma ya elimu karibu na makazi yao, kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule mama ya Maganzo, na kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi wanaotoka maeneo ya jirani.
Mwenge huo umezindua na kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji uliotekelezwa naSerikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kutoka Nyenze hadi Ng’wangh’olo Wilayani Kishapu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa tenki la maji la lita 100,000, vituo vitatu vya kuchotea maji, mtandao wa bomba wa mita 2,670, uzio na alama za bomba, kwa gharama ya Shilingi milioni 445.05 kupitia Programu ya Malipo kwa Matokeo (P for R). Mkandarasi M/s Geo–Spatial Classic Works Ltd kutoka Mwanza ndiye aliyetekeleza mradi huo chini ya usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mradi unatarajiwa kuwahudumia wananchi wapatao 2,345 wa kijiji cha Ng’wangh’olo na maeneo ya jirani kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama, kupunguza magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji machafu, na kuwaongezea muda wa kushiriki shughuli za kijamii na kiuchumi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru umetembelea na kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Wela iliyopo Kata ya Bupigi ikiwa ni zao la jitihada za wananchi waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomita 15 kufuata huduma za afya, ambapo mwaka 2011 walichangisha Shilingi 10,500,000/= kuanzisha ujenzi huo.
Serikali kupitia Serikali Kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri imechangia Shilingi 75,000,000/= kukamilisha ujenzi huo unaojumuisha jengo la zahanati, vyoo matundu matano, kichomea taka na Placenta Pit.
Mradi huu wenye thamani ya Shilingi 85,500,000/= unatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 7,600 wa Kata ya Bupigi na Vijiji jirani, huku ukilenga kusogeza huduma za afya karibu na makazi ya wananchi na kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge amepongeza mshikamano na uzalendo wa wananchi pamoja na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma za afya Vijijini.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 amekagua na kuweweka jiwe la msingi katika bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mwamashele mradi ulianzishwa na wananchi mwaka 2019 kwa lengo la kuwalinda watoto wa kike dhidi ya changamoto za umbali mrefu, mimba za utotoni, unyanyasaji na utoro.
Wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walichangisha zaidi ya Shilingi milioni 25 kuanzisha mradi huo, na Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ilichangia zaidi ya Shilingi milioni 62 kukamilisha ujenzi.
Mradi huu wenye thamani ya Shilingi 88,105,200/= umekamilika na unawanufaisha wanafunzi wa kike 48 wanaolala katika bweni hilo hivyo watoto wa kike wamepata mazingira salama ya kusomea na kuishi shuleni, hatua inayochochea ufaulu na kuimarisha usawa wa kijinsia katika elimu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge amepongeza mshikamano wa wananchi na uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike huku akizindua klabu za kupinga Rushwa na kuzuia ukatili wa Kijinsia.
Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya DED - DC yenye urefu wa kilomita 1 kwa kiwango cha lami nyepesi (DSD), mradi unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 688. Mradi huo unatekelezwa na TARURA kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kuongeza ufanisi wa huduma kwa jamii.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi, amempongeza mwekezaji mzawa Bw. Bin Salum kwa uzalendo wake mkubwa na mchango wake katika maendeleo ya Wilaya ya Kishapu.
Amesema Bin Salum ni mfano wa kuigwa kutokana na uwekezaji mkubwa alioufanya kwa manufaa ya jamii, huku akibainisha kuwa juhudi kama hizo zinaiweka Kishapu katika nafasi ya kuwa Manispaa na hatimaye jiji katika miaka ijayo.
“Bin Salum ameonyesha moyo wa kizalendo kwa kuwekeza fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Huyu ni miongoni mwa wazawa wanaoonesha kwa vitendo kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais katika kuwaletea wananchi maendeleo,” amesema Ussi.
Aidha, amewataka wananchi wa Kishapu kuendelea kumpa ushirikiano mwekezaji huyo na wawekezaji wengine wazawa kwa kuwa mchango wao ni muhimu katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu nchini.
Aidha, Mwenge wa Uhuru umetembelea na kuzindua Klabu ya kuzuia ukatili na Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Mwamashere, ambapo wanafunzi waliwasilisha ujumbe wa kupinga vitendo vya rushwa kwa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu, Tutimize Wajibu Wetu".

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Peter Masindi(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson(Kulia) wakiendelea na ziara ya mwenge wa uhuru Wilayani humo Agosti 8,2025
Katika miradi yote iliyokaguliwa, kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa amesisitiza umuhimu wa usimamizi makini wa miradi ya maendeleo, uwazi na uwajibikaji kwa manufaa ya wananchi.
Mwenge wa uhuru utakabidhiwa kesho Agosti 9,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mhe.Mboni Mhita baada ta kumaliza ziara yake Mkoani Shinyanga katika Kijiji cha Njiapanda kwa ajili ya kuendelea na mbio zake Mkoani Simiyu.

إرسال تعليق