WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAENDELEA KUPATIWA MBINU ZA USALAMA NA ULINZI

 


Mafunzo ya usalama na ulinzi kwa waandishi wa habari yameendelea leo kwa kushirikisha kundi lingine la waandishi wa habari kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), yakilenga kuongeza uelewa juu ya usalama wa kimwili, kidijitali na afya ya akili katika mazingira ya kazi ya uandishi wa habari.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Kadama Malunde, ambaye pia ni mwandishi wa habari, amesisitiza kuwa ulinzi huanzia kwa mwandishi mwenyewe. Ameeleza umuhimu wa kulinda vifaa vya kazi, kutumia nywila imara, kuepuka viunganishi visivyo salama, na kuweka uthibitishaji wa hatua mbili (Two-Factor Authentication), hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mafunzo haya ni sehemu ya mradi wa “Empowering Journalists for Informed Community” unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC), na kutekelezwa na International Media Support (IMS), Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) na JamiiAfrica.

Soma pia : WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAELIMISHWA MBINU ZA KUJILINDA





 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA