
Mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu kutoka Tanzania, Rostam Aziz, anatarajiwa kuzungumza leo kupitia Azam TV (UTV) katika kipindi maalum cha mahojiano.
Kwa mujibu wa tangazo rasmi, mahojiano hayo yatafanyika leo Jumanne, tarehe 2 Septemba 2025 kuanzia saa 3:00 usiku.
Ingawa hakujatolewa dondoo rasmi za mada zitakazojadiliwa, mahojiano haya yanakuja katika kipindi ambacho hivi karibuni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amekuwa akimshambulia Rostam hadharani akimhusisha na tuhuma mbalimbali.
Watazamaji wanatarajiwa kufuatilia kwa karibu kusikia maoni na ufafanuzi wa Rostam kuhusu masuala ya kibiashara, kisiasa na mada moto zinazomhusu.
👉 Usikose kutazama Azam TV leo saa 3:00 usiku.
Post a Comment