MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. PHILIP MPANGO AWASILI NCHINI KENYA KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA KITAIFA YA RAILA ODINGA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 17 Oktoba 2025 amewasili Nairobi nchini Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mazishi ya Kitaifa ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya marehemu Raila Amolo Odinga.


Mazishi ya Kitaifa ya marehemu Raila Odinga yanatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Nyayo, Jijini Nairobi.


Makamu wa Rais ameambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo. 












Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA