

Mtandao maarufu wa uchapishaji na usambazaji wa habari — Malunde 1 Blog — umetwaa tuzo ya heshima ya Best Blogger / Online News Portal katika Mdau Shupavu Awards Shinyanga 2025.
Hafla ya utoaji tuzo imefanyika Ijumaa, tarehe 17 Oktoba 2025 katika Ukumbi wa Zakaria (Miligo Hall) mjini Kahama.
Tuzo hiyo imetolewa na HolySmile Media kwa kutambua mchango mkubwa wa Malunde 1 Blog katika kuelimisha, kuhabarisha na kuchochea maendeleo chanya kupitia maudhui bora ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Mmiliki wa blogu hiyo, Kadama Malunde, ameeleza kuwa ushindi huo ni matokeo ya juhudi, ubunifu na ushirikiano wa wadau wote wanaoendelea kuiamini na kuisapoti Malunde 1 Blog kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

“Tuzo hii si yangu peke yangu, ni yetu sote – wapenzi, wasomaji, na wadau wanaoamini katika nguvu ya habari sahihi, zenye kujenga na kuhamasisha maendeleo. Asanteni sana kwa imani yenu,” amesema Malunde mara baada ya kupokea tuzo hiyo.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa serikali, wafanyabiashara, wanahabari, na taasisi binafsi, huku burudani na vionjo vya Black, Gold & White vikiongeza mvuto wa tukio hilo lenye hadhi ya kipekee.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mdau Shupavu Awards, Arnold Bweichum lengo la tuzo hizo ni “kutambua, kuenzi, na kuhamasisha ubora, ubunifu na ushirikiano katika jamii.”
Mdau Shupavu Awards ni jukwaa maalum la kutambua watu na taasisi mashupavu wanaofanya kazi kwa kujituma na ubunifu, likiwa chachu ya maendeleo endelevu katika mikoa ya Tanzania.

🔵Hongera Malunde Blog – Fahari ya Shinyanga!
#MdauShupavuAwards2025 #MalundeBlog #BestBlogger #Kahama #Shinyanga #HolySmile #TeamMalunde #WadauShupavu








إرسال تعليق