RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA KUINADI ILANI YA CCM KATA YA KIWANGWA

   

📍26 Oktoba, 2025

♻️Kiwangwa, Chalinze 

 🆕Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ameendelea na kampeni za kunadi Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030 katika Kata ya Kiwangwa, akiwataka wananchi kuendeleza imani yao kwa CCM kama chombo kinacholeta maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Katika mkutano uliofurika wananchi wa Kiwangwa, Mheshimiwa Ridhiwani alihimiza umuhimu wa kuichagua CCM katika ngazi zote za uongozi, akibainisha kuwa maendeleo ya kweli hupatikana pale ambapo viongozi wanakuwa na dira moja, moyo wa kujituma, na upendo kwa wananchi.

“Wananchi wenzangu wa Kiwangwa, leo ninawasihi kwa heshima na upendo, tuendelee kuipa kura CCM. Tumpigie kura Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kiongozi mwenye hekima, busara na moyo wa kujali watu. Ameleta mapinduzi makubwa katika nchi yetu elimu bure, afya bora, upatikanaji wa maji, barabara za kisasa, na umeme vijijini. Chini ya uongozi wake, Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo,” alisema Ridhiwani.

Akiwaomba wananchi wamchague tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, amesema kuwa ataendelea kuwa mwakilishi wa kweli wa wananchi na sauti ya maendeleo kwa wote.

“Nimekuwa bega kwa bega nanyi kwa muda wote huu. Najua changamoto zenu, najua ndoto zenu. Naomba kura zenu ili tuendelee kuijenga Chalinze yetu yenye ajira kwa vijana, fursa kwa wanawake, na huduma bora kwa wote. Mimi ni kijana wenu, mwana wenu, na mtumishi wenu. Nikichaguliwa tena, nitazidi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.

Pia aliwaomba wananchi waendelee kuwaunga mkono madiwani wa CCM, akisema wao ni daraja muhimu la kutekeleza sera na miradi ya maendeleo katika ngazi ya kata na vijiji.

“Tuwachague madiwani wetu wa CCM, kwa sababu wao ndio watakaosimamia utekelezaji wa Ilani yetu ya maendeleo. *Tukimchagua diwani wa CCM, mbunge wa CCM na Rais wa CCM – maendeleo yatakuwa ya uhakika. Tukishikamana kama chama na wananchi, hakuna tutakayeshindwa,” alisisitiza Ridhiwani.

Akiendelea kuwahamasisha wananchi, Ridhiwani alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi chake cha uongozi, akisema kwamba ni mfano wa uongozi wa kipekee unaolenga kuleta maendeleo kwa vitendo.

“Dkt. Samia ni mama mwenye maono makubwa na ujasiri, amehakikisha umeme unawafikia zaidi ya asilimia 75 ya vijiji vya Chalinze, maji zaidi ya asilimia 94, elimu bure kwa watoto wetu, na ujenzi wa miundombinu ya kisasa. Ni kiongozi ambaye haongei tu bali anatenda. Ndiyo maana tunapaswa kumpa nafasi ya kuendeleza kazi nzuri aliyoiweka,” alisema Ridhiwani.

Wananchi wa Kiwangwa walijitokeza kwa wingi katika mkutano huo, wakionesha hamasa kubwa, upendo na imani kwa wagombea wa CCM. Wengi walimpongeza Ridhiwani kwa utendaji wake uliotukuka na kumuahidi kumpa kura zote ili aendelee kuwakilisha vyema Jimbo la Chalinze.


#KaziNaUtuTunasongaMbele 🇹🇿
#ChalinzeYaMaendeleo
#CCMInaendeleaKufanyaMamboMakubwa
#RidhiwaniKikweteMitanoTena
#SamiaSuluhuNiKaziNaMatokeoChanya
#UmojaNiNguvuMaendeleoNiUhakika

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA