TUJITOKEZE KUVEMESHA KWA DKT. SAMIA - DKT. DOTO BITEKO



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Doto Mashaka Biteko amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kumchagua mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili Chama hicho kiendelee kuongoza na kuliletea Taifa maendeleo.


Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Oktoba 27, 2025 wakati akihitimisha kampeni za Uchaguzi Mkuu zilizofanyika katika Uwanja wa Kata ya Igulwa, Bukombe, mkoani Geita ambapo amesema wananchi wa Bukombe wana kila sababu ya kujitokeza kupiga kura “Kuvemesha” ifikapo Oktoba 29, 2025.


“ Maendeleo yote katika jimbo letu na maeneo mengine ya nchi ni kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo Dkt. Samia kwa wananchi wake, hivyo tarehe 29 Oktoba 2025 twendeni tukampe kura nyingi za heshima na shukrani kwa mapenzi yake kwetu,” amesema Dkt. Biteko.


Pia amewahimiza wananchi hao wampigie kura za ndiyo  Mgombea wa Ubunge Dkt. Biteko pamoja na madiwani wa CCM ili waendeleze mipango ya maendeleo.


“ Tusibweteke kwa kauli za kutiki bila kujitokeza kupiga kura kwa viongozi watakaoleta maendeleo. Hivyo siku ya Jumatano Oktoba 29, tukapige kura nyingi kwa Dkt. Samia, Wabunge na Madiwani wa CCM na hapo tutakuwa tumetenda haki.” amesisitiza Dkt. Biteko


Aidha, amewashukuru wana Bukombe kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote cha kampeni na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa kulinda na kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.


"Nataka niwaambie wana Bukombe huwa mnanipa deni kubwa sana moyoni mwangu hamjui tu, huwa hamjui huwa najiona mmenipa stahili nisiyostahili kwa sababu kama binadamu nina mapungufu yangu mengi lakini mnanipa heshima,” amebainisha Dkt. Biteko


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Geita, Nicholous Kasendamila amehimiza wananchi wa Mkoa huo kutumia haki yao ya Kidemokrasia na kujitokeza kupiga kura. “ Kazi ya kampeni iliyodumu kwa takribani miezi miwili haitakuwa na maana endapo hatutajitokeza kupiga kura.”  


Kampeni hizo za Urais, Ubunge na Udiwani kwa Jimbo la Geita zilizinduliwa Septemba 2, 2025 ambapo Kampeni za kitaifa zitahitimishwa siku ya Jumanne Oktoba 28, 2025 katika Uwanja wa Kirumba, mkoani Mwanza.





Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA