TUNATAKA UCHAGUZI WA UHURU NA AMANI, MFIKISHIENI SALAMU


Na, Mwandishi wetu Fichuzi news blog.

Hali ya kisiasa katika Jimbo la Hai imechukua sura mpya baada ya Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Saashisha Mafuwe, kueleza kutoridhishwa kwake na kauli za mpinzani wake wa kisiasa, Mbowe James anayewania ubunge kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).


Mafuwe amedai kuwa kauli hizo, ambazo zilitolewa kwenye moja ya mikutano ya kampeni, zinaashiria kejeli dhidi ya Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jambo alilolitafsiri kama kukosa heshima kwa viongozi wa kitaifa.


Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Ijumaa, Oktoba 17, 2025, katika Kijiji cha Lyamungo, Machame Mashariki, Mafuwe alisema si sahihi kwa wanasiasa kutumia kampeni kama jukwaa la kubeza au kudhalilisha viongozi "Siasa si uwanja wa kejeli wala uongo, tunapaswa kuendesha kampeni zenye hoja, sera na heshima kwa viongozi wetu,” alisema Mafuwe huku akishangiliwa na wananchi pamoja na wafuasi wa CCM waliohudhuria mkutano huo."


Katibu wa CCM Wilaya ya Hai Mkaruka Kura, alilaani kauli hizo na kueleza kuwa mgombea wa upinzani amewapotosha wananchi wa 'Kwasadala' kwa kudai mgombea wa CCM alimdanganya kiongozi wa nchi kuhusu fedha za soko, ilhali fedha hizo zilishatolewa na mkataba wa ujenzi ulisainiwa siku iliyofuata, jambo linaloonesha kuwa tuhuma hizo hazina ukweli.


"Ni vyema wanasiasa wakawa wa kweli kwa wananchi, Kauli za upotoshaji hazijengi taifa bali zinachochea chuki,” alisema Kura.


Katika mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Chama hicho akiwemo Mhe. Ummy Hamis Nderiananga ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) amemnadi mbunge Saashisha kuwa ni kati ya wabunge imara, makini, anayejenga hoja na kuwatetea wananchi wake na kuwataka wananchi hao wasifanye makosa badaa yake waendelee na imani hiyohiyo, muda huo huo Salome Makamba akaibuka kuomba  kura ya urais kwa Dkt. Samia, na ubunge kwa Mhe. Mafuwe na kusisitiza wananchi wasidanganyike kwa kukaa usingizini badala yake waamke kwa maendeleo ya Hai.

Mafuwe ameendelea kuwataka wananchi wa Jimbo la Hai kuzingatia amani, umoja na kuepuka siasa za matusi, akibainisha kuwa malengo yake ni kuwaletea maendeleo kupitia utekelezaji wa sera za CCM.

"Hatakiwi kumkashfu Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta maendeleo makubwa kwa kipindi cha miaka mitano, Mama huyu ametupa heshima ndani ya Wilaya hii na wananchi wa Hai hawawezi kukubali matusi au dhihaka dhidi ya maendeleo haya, Namsihi James aache mara moja kumtukana mgombea wetu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi." Alisema Mafuwe

Hadi kufikia sasa, kampeni za ubunge katika Jimbo la Hai zimeendelea kwa amani, ingawa kauli na mikwaruzano ya kisiasa imekuwa ikizua mijadala katika mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara.
















Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA