VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

 



Na Mwandishi wetu, Mbeya

Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na watu Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga, amewataka vijana kote nchini Tanzania kutumia haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaoakisi matumaini, malengo na ndoto za taifa la Tanzania katika kipindi cha mitano ijayo.

Walakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vijana Tanzania linalofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa City Park Garden, Jijini Mbeya na kuhudhuriwa na Vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini, Maganga amesema vijana wana nafasi kubwa katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, hivyo ni muhimu wakatumia fursa hiyo kuchagua viongozi wanaolenga ustawi wa taifa.

“Vijana ni nguvu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii zetu, Hivyo ni lazima tutumie vyema nguvu hii kubadilisha dunia kuwa mahali bora kwaajili ya watu wote. Hivyo, ninawasihi mjitokeze kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, na kuchagua viongozi wenye dira sahihi kwa taifa letu,” amesema Bi. Maganga.

Katibu Mkuu huyo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea pia ya kuweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha vijana, ikiwamo mifumo ya kisera, kisheria, Kitaasisi pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa Mikopo na usaidizi mwingine unayolenga kuongeza ushiriki wao katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Ameongeza kuwa kongamano hilo ni jukwaa muhimu kwa vijana wa Kitanzania kubadilishana mawazo, kujifunza na kujadili changamoto zinazowakabili, ili serikali iweze kuyatumia maoni yao katika kuboresha sera na miongozo ya vijana nchini.

Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Rodrick Mpogolo, amewataka vijana kuendelea kuwa wazalendo na kujivunia taifa lao, akisema mchango wao ni muhimu katika kulijenga taifa lenye misingi imara ya maendeleo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Seleman Mvunye, amesema kongamano hilo limewakutanisha zaidi ya vijana 1,500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA