WAZIRI NDEJEMBI AKABIDHIWA OFISI NA ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI DKT. BITEKO




Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo 20 Novemba, 2025 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko kwenye ofisi za Wizara zilizoko mtumba mkoani Dodoma, na kumshukuru Mhe. Biteko kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake.


Waziri Ndejembi amesema katika kipindi cha uongozi wake, utendaji kwenye sekta ya nishati umekuwa kwa kiasi kikubwa na huduma za utendaji zimeboreshwa na tija kuonekana katika harakati za kukuza sekta ya nishati.


Waziri Ndejembi ameahidi atayaendeleza yote pale alipoishia Mhe.Biteko, ili kuhakikisha azma ya serikali na maono iliyonayo kufanikisha miradi ifikapo 2030 yanafikiwa.


Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Biteko amempongeza Mhe. Deogratius Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na kumhakikishia kumpa ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono makubwa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Nishati.


 “ Mengi niliyojifunza kipindi nikiwa Wizara ya Nishati lakini jambo kubwa zaidi ni sala zangu kwenu katika utekelezaji wa kazi zenu za kila siku “ amesema Biteko. 


Halfla ya Makabidhiano hayo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati.










Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA