DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA BANDARI YA UVUVI, KILWA.


-Asema Rais Dkt. Samia ni kiongozi anayetekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania_.


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba  leo Desemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi iliyopo Kilwa Mkoani Lindi.


Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Dkt. Mwigulu amesema kuwa bandari hiyo ni mojawapo ya miradi mingi inayofafanua kauli za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  alizozitoa baada ya kuapishwa za kusimamia utekelezaji wa miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania.


Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato na kubadili maisha ya Mtanzania pamoja na kuongeza pato la Taifa. “Rais Dkt. Samia ni kiongozi ambaye anatekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za watanzania”


Ameongeza kuwa ili kuhakikisha mradi huo unafanya vizuri Rais Dkt. Samia amehidi kununua meli 5 za uvuvi. “Tanzania inakwenda kuandika historia mpya kwenye sekta ya uvuvi, Rais Dkt. Samia aliahidi kuendeleza miradi iliyoanzishwa na watangizi wake na mmoja wapo ni wa Bandari ya Uvuvi  iliyopo wilayani Kilwa.


Mradi huo ambao umefikia asilimia 90 ya ujenzi wake umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 280.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA