JESHI LA POLISI LAWANYOOSHEA KIDOLE WANAOPANGA TENA MAANDAMANO BAADA YA KUTOFANIKIWA JANA

 
Na, Mwandishi wetu - Fichuzi news blog.

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa onyo kwa watu wote wanaodaiwa kupanga kufanya maandamano ya amani yasiyokuwa na kikomo, ambayo yalipangwa kuanza kufanyika jana Jumanne Desemba 9, 2025. Maandamano hayo yaliyopigwa marufuku tangu Desemba 5 kwa sababu ya kukosa sifa za kisheria na yalishindwa kuendelea jana baada ya ulinzi kuimarishwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mapema Leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania David Misime akitoa taarifa ya mwenendo wa hali ya ulinzi na usalama nchini ametoa onyo kali kwa wale wanaopanga kutekeleza maandamano hayo leo, Desemba 10, 2025 na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kuyafanya hivyo ikizingatiwa kuwa tayari yalipigwa marufuku mapema wiki hii.

Taarifa hiyo inakuja baada ya hatua na maonyo yaliyotolewa awali, kabla ya uamuzi wa Desemba 5 wa kupiga marufuku maandamano hayo.

Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, aliwashukuru Watanzania kwa kuonyesha utulivu na uzalendo katika kuilinda amani ya Tanzania wakati Taifa likiadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi, baada ya maandamano hayo yasiyokuwa na kikomo kukwama Desemba 9, inadaiwa watu hao wamepanga kuyafanya leo Jumatano Desemba 10,2025.Hata hivyo, mkazo wa Jeshi la Polisi ni kuwa maandamano yasiyopangwa kwa mujibu wa sheria hayataruhusiwa na kwamba watakaojaribu kuvunja amani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA