Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia msiba wa aliyewahi kuwa Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kufuatia taarifa iliyotolewa leo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu
"Nimepokea
kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho,
Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama. Ninatoa pole kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, wananchi
wa Jimbo la Peramiho, familia, ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa
miaka 38, Mheshimiwa Mhagama amekuwa mwanachama mahiri wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kiongozi wa vijana, kiongozi wa wanawake, waziri katika
awamu mbalimbali na mnasihi wa wengi katika siasa na maisha.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Amina." Dkt. Samia
Post a Comment