Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kenani Kihongosi ametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Barabara ya Kitukutu–Msingi, inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Amefanya ukaguzi huo leo Januari 21, 2026 ikiwa ni sehemu ya ziara yake Iramba Mkoani Singida
Barabara hiyo itakayounganisha Mkoa wa Singida na Simiyu inatarajiwa kufungua fursa muhimu za kiuchumi katika Kanda ya Ziwa pamoja na Kanda ya Kati, ikirahisisha usafiri na kuongeza ufanisi wa biashara.
Mradi huo unagharimu zaidi ya Sh. Bilioni 9, ambapo hadi sasa Sh. Bilioni 2 tayari zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kihongosi amemtaka Mkandarasi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kuzingatia viwango vinavyolingana na thamani ya fedha zinazowekezwa, ili wananchi wanufaike ipasavyo na mradi huo wa kimkakati.
Habarika & Burudika
إرسال تعليق