MAGANGILA AITAKA SERIKALI KUONGEZA UTAFITI KUZAA MIGODI MIKUBWA

 

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, akichangia mjadala wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13, amesema Serikali inapaswa kukaa pamoja na wawekezaji na wachimbaji wadogo ili kufanya tafiti mpya zitakazozaa migodi mikubwa badala ya kutegemea migodi iliyofanyiwa utafiti miaka mingi iliyopita.


Magangila amesema lengo la Serikali linapaswa kuwa ni kupanua wigo wa sekta ya madini kwa kuongeza utafiti na vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi ili kuvutia makampuni mengi ya utafiti.


 Akibainisha kuwa baadhi ya wamiliki wa leseni kubwa za utafiti wameacha kufanya tafiti jambo linalokwamisha upatikanaji wa migodi mipya mikubwa.


“Tumeweza kuanzisha migodi mipya lakini ni migodi ambayo imefanyiwa utafiti miaka mingi nyuma. Twendeni sasa kupitia Wizara yetu ya Madini, Mhe. Rais amekusudia vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi ili kukuza sekta binafsi. Twendeni tukaweke vivutio hivyo, tukaongeze utafiti na makampuni mengi ya utafiti hasa yanayomiliki leseni kubwa za utafiti yaliacha kutafiti, na tunapoacha kutafiti tunaua matarajio ya kuwa na migodi mingine mikubwa kama Geita, Barrick, North Mara, Bulyanhulu ambayo ilitafitiwa miaka mingi nyuma. 

Twendeni tukakae na hawa wawekezaji tuangalie ni namna gani tutawavutia watafiti migodi mingine”Mabula Magangila – Mbunge wa Jimbo la Msalala.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA