Na, Mwandishi wetu.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji (OR-MU), Mhe. Dkt. Pius Chaya, amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Gatsby Africa, Bw. Justin Highstead, Januari 22, 2026, jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kiufundi utakaochechemua ufanisi katika sekta ya mipango na uwekezaji nchini.
Dkt. Chaya ameipongeza Gatsby Africa kwa kuwa mshirika imara katika utekelezaji wa programu mbalimbali za maendeleo zinazoongozwa na Ofisi ya Rais, mipango na uwekezaji.
Kwa upande wake Bw. Highstead amesisitiza utayari wa Gatsby kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali, akisifu mazingira wezeshi na utayari wa OR-MU katika kurahisisha utekelezaji wa miradi ya pamoja.
Post a Comment