Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, leo tarehe 20 Januari, 2025, amefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hatua za Serikali katika kuboresha huduma za bandari.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwasiliana moja kwa moja kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, kwa lengo la kuimarisha uwazi, uwajibikaji na uelewa wa umma kuhusu kazi za Serikali.
Post a Comment